top of page

Unabii 21 “Pale NDIMI NILIYE YUPO, Ndipo Pale Pasaka Yako Itakuwa!”

Updated: Apr 14


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 15 Machi, 2019





Maandiko Husika


1 Petro 5:8-11: “Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza. Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kwamba mateso kama hayo yanawapata ndugu zenu pote duniani. Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, MUNGU wa neema yote, Aliyewaita kuingia katika utukufu WAKE wa milele ndani ya MASHIAKH YESHUA, YEYE MWENYEWE Atawarejesha na kuwatia nguvu, Akiwaimarisha na kuwathibitisha. KWAKE uwe utukufu na mamlaka milele na milele. Amen.”


1 Wathesalonike 5:5-8: “Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku. Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine walalavyo, bali tukeshe na kuwa na kiasi. Kwa kuwa wote walalao hulala usiku na wale walewao hulewa usiku. Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo.


Tito 2:11-13: “Kwa maana neema ya MUNGU ambayo inawaokoa wanadamu wote imefunuliwa. Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa, huku tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa MUNGU wetu Mkuu, Aliye Mwokozi wetu YESHUA HAMASHIAKH.”



Ujumbe wa Kinabii


Mnaingia sasa katika nyakati za huzuni, siku za huzuni, majaribu ya ole na maombolezo makubwa. Kiza! Kiza! Kiza kinafunika nchi – kuzuka kulikomo ndani ya moyo wa mwanadamu – huzuni, simanzi, maombolezo, na kutaabika kukuu.


Ee binadamu, ni nini ambacho mko karibu kuzaa? Ni uovu upi huu ambao mmetunga katika utundu, katika kiza cha weusi cha akili zenu, mioyo yenu? Sikuwaumba kuwa kama vyombo vya utupu, vya kufa moyo na [vya] giza. Ole wenu! Ole wenu! Ole na iwe kwa wanadamu na vizazi vyao!


Kuna utulivu katika roho – huzuni wa moyo, uzito, uzito mkubwa. Mmesimama kwenye ukingo wa mwamba. Je, mtapuruka? Je, mtapaa? Au je, mtaanguka? Mwanguko mkubwa, uasi mkubwa. Kama vile ilikuwa mbeleni katika mwanzo, hivyo pia itakuwa mwishoni, lakini kumbuka, Watoto WANGU, Nafanya mambo yote mapya.


NInaruhusu dhambi kufanyika vile imefanyika kufundisha binadamu, kuonyesha binadamu uasi haufaidi. Sio sasa, wala daima. Ulichukua mtego wa shetani na ukajivisha. Oh yale machukizo makuu yamefanywa katika jina la sayansi! Binadamu, mlicheza moja kwa moja [hadi] mtego wa shetani. anacheza nanyi, anawachezea, anawachukia. Chuki yake kwenu imefungwa katika kifurushi kizuri. Kwa maana kwani yeye haji, wahudumu wake kwani hawaji kama malaika, wajumbe wa mwangaza?


Na bado, Nawaambia, kiza kikuu kabisa chaja katika umbo la ukweli, katika umbo la Utaua lakini hakuna chochote takatifu, hakuna chochote CHANGU – ABBA wenu YEHOVAH, YESHUA wenu – kinachopatikana ndani yake. Oh nyakati za udanganyifu mkubwa mnazoishi ndani yake! Hakuna kinachoonekana kilivyo! Hakuna kinachoonekana kilivyo!


NIsikieni Watoto WANGU! Huu ni wakati ambapo kiasi kikubwa [kunahitajika], kuwa macho pakubwa panahitajika. Kwa huzuni, wengi watafagiliwa mbali na mawimbi ya bahari, gharika la uongo katika uovu. Natikisa kichwa CHANGU katika huzuni, simanzi. Hizi si nyakati nzuri. Nahitaji kuwaambia, Watoto WANGU, uhalisia wa vitu ili msishikwe ghafla [katika kutojua], ili msiwe na mwamsho wa kushtuliwa.


Watoto WANGU, kuweni wenye moyo mwepesi, naam, lakini msiwe wazembe. Raha ya mwili hupelekea ufukara, lakini nidhamu huzaa maisha na huruma nyororo. MsiNIjaribu, Watoto WANGU. Hizi ni nyakati nzito, nyakati za vita. Tamanio LANGU ni kulinda, kukinga, kupandisha cheo. MIMI Najihusisha na shughuli YANGU. Je, nawe [wajihusisha nayo]? Nawapenda Watoto WANGU. Ndiyo, MIMI, BABA yenu YEHOVAH, Nawapenda na upendo [ambao] hamuwezi fahamu.


DAMU ya YESHUA – ikiwa kungekuwa na kafara ya kinywaji bora zaidi, NIngepeana. Watoto WANGU, Watoto WANGU njooni kwa PAPA. Acheni NIwakumbatie, NIwashike (kabisa) kwa nguvu. Msikwepe mguso WANGU Mtakatifu, kinga ya mabawa YANGU ya Zaburi 91. Hakuna kwa hakika Kimbilio Salama lingine ila MIMI, ila MIMI, YEHOVAH. Pale NDIMI NILIYE YUKO, ndipo pale Pasaka yenu itakuwa. Kuwa pale NIKO. Kuweni Watakatifu kama NDIMI NILIYE Alivyo Mtakatifu (1 Petro 1:16). Mnajua Maandiko, sasa yahubiri, yaishi. NDIMI NILIYE YUKO nanyi hata hadi mwisho wa nyakati, pale wale wenye nguvu wa Mbinguni, wa vitu asili watatikiswa.



Mwisho wa Neno

3 views

Recent Posts

See All
bottom of page