top of page

Unabii 48 “NInaita Makabila Yaliyopotea ya Israeli!”

Updated: Mar 24


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 9 Julai, 2019


Maandiko Husika


Yeremia 23:7-8: “Hivyo basi, siku zinakuja,” Asema YEHOVAH, “wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama YEHOVAH Aishivyo, Aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ bali watasema, ‘Hakika kama YEHOVAH Aishivyo, Aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote Alizokuwa Amewafukuzia.’ Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”


Hesabu 11:23: “Na YEHOVAH Akamjibu Musa, ‘Je, mkono wa YEHOVAH umefupishwa? Sasa utaona kama jambo NIlilolisema litatimizwa juu yako au la.”


Isaya 59:1: “Hakika mkono wa YEHOVAH si mfupi hata usiweze kuokoa, wala sikio LAKE si zito hata lisiweze kusikia.”


Ujumbe wa Kinabii


Ee, NInaita Makabila Yaliyopotea – hayajapotea KWANGU, lakini kwa wao wenyewe, kwa sababu kupitia dhambi walisahau utambulisho wao (Yeremia 23:7-8). Lakini NItarejesha, NItafanya mpya, wanapokuja mmoja mmoja mbele YANGU, “NDIMI NILIYE” Mkuu, kwa magoti yaliyoinama katika unyenyekevu, na uraruaji mkubwa wa moyo; NInapoinua shela ya laana ya kutoNItii.


Kwa maana wakati huNItii, unapopotoka, wakati yeyote anapotoka – wanapoteza mwelekeo, wanapoteza fokasi ya MIMI,YEHOVAH, na kwa sababu hiyo [wanapoteza pia] wao ni nani ndani YANGU. Makabila yote, ikijumuisha Yuda, wamepoteza mwelekeo, hawajakuwa watiifu.


Lakini NItafanya marekebisho. NItarudisha yale yaliyokuwa, njia za kale. NItainua mipaka ya makabila, migao ya kale – kila kitu katika wakati, msimu, na utaratibu wake kamili. NInangoja tu wakati WANGU kamili, utaratibu WANGU kudhihirika. Saa inapogonga saa sita (usiku), tazama na muone UTUKUFU WANGU ukidhihirika. Tazama na muone NIkifanya kazi ya upesi Duniani kwa ajili ya Wateule WANGU (Mathayo 24:222). Mafumbo mengi yatakuja tukia.


Ee Israeli, MIMI, YEHOVAH, Nawapenda. Nawanyoshea mkono. Mkono WANGU si mfupi mno hadi kwamba hauwezi okoa (Hesabu 11:23, Isaya 59:1). NIlivyowaokoa katika siku za Misri wakati wa Moshe, vivyo hivyo pia nguvu zinabaki sawa, zinaokoa leo. Kwa maana, je MIMI si yule yule jana, leo na milele zaidi?


MIMI, YESHUA, sasa Nazungumza. Ni mikono YANGU iliyonyooshwa pale Kalivari ambayo itawaokoa tena, ee Israeli. JINA LANGU, Nguvu ZANGU, Damu YANGU haitawahi poteza nguvu, haitafifia kamwe, haitafifiliza kamwe. Kwa maana upendo WANGU, ua la upendo WANGU, kamwe haufifii. MIMI ni YULE YULE jana, leo na milele (Waebrania 13:8). Ee Israeli, NIsikieni! MIMI, YESHUA, Nawapenda. Ndiyo, Nawakemea, kwa maana Sifai NIwakosoe katika makosa ya njia yenu? Haifai NIdhihirishe upendo WANGU kwenu? NInakosoa yule Nataka. NInafundisha mtoto katika Njia anapaswa kuenda (Mithali 22:6).


Itaendelezwa

5 views

Recent Posts

See All
bottom of page