Unabii 57 “Msikawie Katika Kufanya Kazi YANGU,” Asema MIMI, YEHOVAH!
Updated: Mar 25
Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umepokewa 9 Oktoba, 2019
Maandiko Husika
Yeremia 18:6
“Ee nyumba ya Israeli, je, SIwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” Asema YEHOVAH. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono WANGU, ee nyumba ya Israeli.”
Isaya 53:2
Maana Atakua (YESHUA) mbele YAKE (YEHOVAH) kama mche mwororo
Na kama mzizi katika nchi kavu.
HAna uzuri wala utukufu wa kutuvutia KWAKE,
HAna chochote katika sura YAKE cha kutufanya tuMtamani.
Je, si MIMI Humba? Si NInaambia udongo wa mfinyanzi na inakuwa hivyo? NInafanya umbo. NInavunja. NInafanya umbo upya. UsiNItie shaka MIMI, MUUMBA.
NIkikuweka mahali, unapaswa kusitawi. Unapaswa kuchanua na kutoa maua. Je, MIMI YEHOVAH, si NIlipanda MWANANGU YESHUA mahali pagumu kabisa, pakavu kabisa? Kama mzizi kutoka ardhi kavu Alichomoza (Isaya 53:2). Kwa kweli Alichanua na kutoa maua.
Alikomaa na mwanadamu na MUNGU. NIlimwaga juu YAKE ROHO WANGU, RUAKH HAKODESH WANGU MTAKATIFU (Luka 2:40,52). Alitembea katika njia ZANGU na bila kuchelewa. Alihimiza na udharura ili kazi YANGU ipate kufanyika.
Hakukawia au kugeuka kulia au kushoto. MWANANGU ambaYE NIlituma Alitimiza mapenzi YANGU kikamilifu. Hiyo ndiyo maana mna upatanisho wa DAMU. Hiyo ndiyo maana mna Wokovu. Katika kuteseka AliNIpa UTUKUFU. Ukiteseka naYE, utatawala naYE pia (2 Timotheo 2:12).
Fuata mfano wa MWANANGU YESHUA. Aliweka wazi Torah mbele zenu. Aliifanya rahisi na wazi. Tembeeni kwa imani na hamtadanganyika. Kuna walaghai wengi wanaotembea katika nchi. Lakini ukitembea kwa imani na kuchukua Neno LANGU lilivyo, lionekanavyo kijuu juu, hautakosea. Usichelewe katika kutimiza kazi YANGU (Waefeso 5:15-16).
Lazima NIwavue nguvu zenu za kimwili ili mweze kupeperuka juu, juu zaidi katika upako. Mchakato huu si raha, lakini lini hii ikawahi kuhusu kuburudishwa? MIMI, YEHOVAH, SIfanyi mzaha, SIjawahi. Ndio, Nafurahi kukaa na kila mmoja wenu na kuwaona mkicheka lakini hizi ni nyakati nzito. Nafsi zimo hatarini. YESHUA Alikuja kufanya Mapenzi ya BABA. Alifanya tu kile AliNIona NIkifanya. Hiyo ndiyo maana YEYE pia Hakuwa katika biashara ya kuburudisha. Alikuja kuJIhusisha na kazi ya BABA YAKE. Kazi ya BABA YAKE ni utaratibu, sheria na utaratibu.
Mko sasa mbele ZANGU, katika uwepo wa MFALME (Zaburi 95:6). Kila mfalme ana utaratibu. Kila ufalme una itifaki. Duniani kama ilivyo Mbinguni. NImewaonyesha itifaki YANGU, Sheira na Utaratibu WANGU. Haki ni YANGU. Rehema ni YANGU. Katika Mkono WANGU wa Kulia kuna Wokovu. Nuru ya Wajihi ni maisha marefu. Katika Uwepo WANGU kuna utimilifu wa furaha namaagizo ya milele. MIMI ni YEHOVAH MFALME wenu, NIkitawala na rehema na ukweli (Zaburi 89:14).
Uhai unatoka kwa Kiti CHANGU cha Enzi. Kukataa utawala WANGU ni kutafuta mauti na utarithi malipo yake (Warumi 6:23). Msifikiri mnaweza kwepa kwa njia zenu. Njia zenu huelekeza kwa umaskini, lakini ZANGU kwa uzima wa milele. Malipo ya utiifu ni uzima milele zaidi. Unatuzwa kulingana na chaguo lako. Kuna matokeo kwa kila uamuzi. Chagua kwa hekima na utaishi. NIchague MIMI na SItawahi kuwacha au kukutelekeza (Waebrania 13:5).
Torah YANGU haina miaka (Isaya 40:8). Haijafungwa na vifungo vya mwanadamu. MIMI ni YEHOVAH WA MILELE.
Comentarios