top of page

Unabii 31“Njooni KWANGU – Mwito wa Hukumu!”


Umepewa Nabii Shema’YAH kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 19 Machi, 2019

Maandiko Husika


Mathayo 5:14-16 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya ile nyumba. Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema waMtukuze BABA yenu Aliye Mbinguni.”

Yoeli 2:1-3 “Pigeni tarumbeta katika Sayuni; pigeni mbiu katika Mlima WANGU Mtakatifu. Wote waishio katika nchi na watetemeke, kwa kuwa siku ya YAHUVEH inakuja. Iko karibu, siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na utusitusi. Kama mapambazuko yasambaavyo toka upande huu wa milima hata upande mwingine jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja. Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani wala halitakuwepo tena kamwe kwa vizazi vijavyo. Mbele yao moto unateketeza, nyuma yao miali ya moto inawaka kwa nguvu. Mbele yao nchi iko kama Bustani ya Edeni, nyuma yao ni jangwa lisilofaa: hakuna kitu kinachowaepuka.”

Ufunuo 6:7-8 “Alipovunja ile lakiri ya nne, nikasikia sauti ya yule kiumbe wa nne mwenye uhai ikisema, “Njoo!” Nikatazama, na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mwenye rangi ya kijivujivu! Yeye aliyempanda aliitwa Mauti, naye Kuzimu alikuwa akimfuata nyuma yake kwa karibu. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.”

Isaya 60:1-5 “Inuka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa YAHUVEH umezuka juu yako! Tazama, giza litaifunika dunia na giza kuu litayafunika mataifa, lakini YAHUVEH Atazuka juu yako na Utukufu WAKE utaonekana juu yako. Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako. “Inua macho yako na utazame pande zote: Wote wanakusanyika na kukujia, wana wako wanakuja toka mbali, nao binti zako wanabebwa mikononi. Ndipo utatazama na kutiwa nuru, moyo wako utasisimka na kujaa furaha, mali zilizo baharini zitaletwa kwako, utajiri wa mataifa utakujilia.”

Ujumbe wa Kinabii


SIdanganyi. Nyinyi ni wa dhati sana KWANGU!

Kanisa halitaamini NInakuja. Wanafikiri Niko mbali. Oh, lakini jinsi walivyo makosa. Watashangaa wakati ghafla NItafika kwa Hekalu LANGU. Huu moto NInaowapa utakataliwa na wengi. Wangi watachomwa. Wachache wataokolewa.

NInawategemea nyinyi nyote kushiriki maarifa yale ambayo NImewapa. Songeni haraka, kwa maana wakati ni mfupi. Hakuna kukawia tena. Andika, taipu upesi. Lisheni Watu WANGU. Yatoeni, Maneno [haya], nje – upesi. Watapotea bila nuru yenu. Ng’aaeni kwa ung’avu ili wote waone (Mathayo 5:14-16).

NIsikie, hizi siku ndizo za mwisho. Wokovu uko kwenye mlango (2 Wakorintho 6:2). Adhabu ya kutengwa na ELOHIM iko pale pale nyuma yake. Naja upesi. Neema haikai milele. NIimbie katika hizi Siku (nyakati) za Mwisho, [kwa maana] MIMI ni kimbilio lenu (Zaburi 91:1-16).

NItawaokoa katika hizi Siku za Mwisho. Kiza kikuu kinavyokuja, jua NItakuokoa (Yoeli 2:1-3). Nyinyi ni Mpendwa WANGU. NYINYI ni Kondoo WANGU na MIMI ni MCHUNGAJI wenu. Na SIachi Kondoo. NInakusanya Kondoo WANGU wote kutoka kona nne za dunia!

Watoto WANGU njooni KWANGU. Njooni KWANGU. NInawaita! Wale 144,000, njooni! NInawaita Watoto WANGU – Ninawaita, Watoto WANGU wote! Kutoka kila sehemu ya dunia! Njooni! Njooni KWANGU! NItawaponya! NItawaokoa! Kwani, hamwezi NIsikia NIkiwatwetea?

Kwa maana mapigo makubwa yanakuja kwenye hii dunia. Na ikiwa hamtageuka kutoka kwa njia zenu zenye uvunjaji Sheria, mtashikwa kati kati yake. Na hamtaki kuwa pale. Oh, hamtaki kuwa pale! Je, hamwezi NIsikia NIkilia? Mnapoangalia kote kando yenu na mauti ndiyo yote mnayoona – oh, hamtaki kuwa pale! Huyu Kondoo WANGU Natumia kuzungumza, kuwafikia. Na EZRA WANGU, AmbaYE ndiYE MCHUNGAJI MKUU Anawaombea.


Hakuna muda zaidi. Mauti yanasongea karibu na Kuzimu nayo (Ufunuo 6:7-8). Watu WANGU, NIsikieni! Mnafaa kuishi katika hii dunia lakini kutokuwa kama hii dunia, kutokuwa wa hii dunia. NIrudieni! NIrudieni! Nyinyi ni nani? Mnafikiri nyinyi ni nani kuNIkana? Nirudieni! NInawaita.

Watoto WANGU, moyo WANGU unawalilia, unawatwetea, unawalilia! Kile maadui wanaenda kufanya, kujaribu kufanya… Njooni katika ulinganisho! Njooni katika ulinganisho! Kuweni Watakatifu kama vile NDIMI NILIYE Alivyo Mtakatifu (1 Petro 1:16)! Huu ni wakati wa mwisho NInawaita. NInakuja kuokoa Watoto WANGU.Lakini lazima mNIsikie kwa dhahiri: hakuna dhambi zaidi!!!


MIMI ni MTAKATIFU! MIMI ni MWENYEZI MUNGU! YAHUSHUA HAMASHIACH! MWOKOZI wa pekee wa dunia! Kwa hivyo msisikize yeyote mwingine! Kwa sababu NIlilipa Gharama! Na MIMI NDIYE MCHUNGAJI MWEMA (Yohana 10:1-11). Na NInakuja kuokoa Watu WANGU, Watoto WANGU.

Lakini mna njia ngumu ya kusafiri kwa ajili ya kutotii kwenu. Kwa ajili ya kutotii kwenu!

Kwa hivyo NIsikieni sasa. Hii dunia inakuja kuisha. Na SIsubiri tena! Kwa maana MIMI NI MUNGU MWEZA! MIMI NDIYE MFALME! Na mnakuja KWANGU NInapoita! MIMI NI BWANA wa Ulimwengu! MFALME juu ya wote Watakatifu!


Watoto WANGU, NIfurahisheni. Angukeni kwenye magoti yenu na mtubu mbele ZANGU. Kwa maana Naja upesi na hakuna kukawia tena! Kwa hivyo msisimame. Angukeni kwenye magoti yenu na mje mkikimbia KWANGU MIMI. NItawaponya. NItaondoa uchungu. NItawaponya. NItawaokoa na kuwahifadhi. Lazima mNIsikie. Nazungumza na roho zenu, ambazo NIlijua kabla ya msingi wa hii dunia. Kwa hivyo, njooni mkiNIkimbilia, kwa maana muda unaisha. Muda unayoyoma. Yay, na hakuna muda zaidi. Maana kwa muda gani mtafanya NIngoje? Na MIMI NDIYE MFALME.

NInawajali Watoto WANGU. NInawapenda. Na sasa ni wakati wenu wa kuNIpenda.


Mwisho wa Neno


2 views

Recent Posts

See All
bottom of page