top of page

Unabii 39“Uvundo wa Marekani Umefika Mbinguni!”

Updated: Jan 26, 2021

Umepewa Nabii Shimshon kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa Aprili 12, 2019

Ujumbe wa Kinabii

NIna mengi ya kusema! NIna mengi ya kusema, MwanaNGU, maana SIkusema – uvundo umefika Mbinguni? Uvundo wa Marekani, uvundo wa nchi zote za hii dunia, kutoka kwa bahari hadi bahari! Hizi nchi ovu, NInawadharau! HamNIfahamu.


Je, SIkusema, mtaona MWANA wa Adamu Akipanda mawingu ya Mbinguni? Kwa nini? Kuleta hukumu na ghadhabu iteketezayo! Hakuna mmoja wenu anayejua – kizao hiki, kiwe ni tajiri au maskini – hamfahamu vita. Ni zaidi ya mchezo wa video. Ni zaidi ya yale mnayosoma katika habari. Hata mnaposikia kuhusu vita, mataifa jirani, Marekani yaendelea kubaki katika njozia mataifa mengi ya hii dunia.


Vipofu kabisa, hawana dhana ya uhalisi. Hawaamini hata katika vita. Kwa hivyo wako vipofu kabisa kwa vile vita vinavyokuja kutoka Mbinguni. Isipokuwa wachache WANGU kote duniani, ambao wana moyo WANGU, moyo wa MIMI, YEHOVAH. Mtaishi, NItawachukua, au NItawalinda.


Na NIna baadhi, maana, ingawa Nawapenda, itawabidi wateseke kwa sababu ya kutotii. WanaMsikiza Nabii WANGU? WanaMsikiza Mjumbe WANGU? Kwa hivyo NInawatuma, nyinyi Wana na Mabinti WANGU waaminifu, Wana na Mabinti WANGU Waliodhihirika!


NInawatuma kama kiwango dhidi ya uovu. Wanaamini sana kwamba watakuja ndani kama mafuriko na kugharikisha dunia. Wanafikiri watakuja ndani kama mafuriko na kuvunja milango ya Mbinguni. Wapumbavu, wanaume wapumbavu, wanawake wapumbavu! Tayari NIshainuka juu ya kiwango kwa vile nyinyi nyote ni Wana na Mabinti WANGU waliodhihirika wa BiArusi WANGU.

Na dunia itafahamu nani ni Wana na Mabinti Wa MWENYEZI MUNGU Waliodhihirika! Watagundua, upepo utagundua, nchi! Ndiyo – upepo una sauti, nchi/ardhi ina sauti, maji yana sauti, radi ina sauti – zitawasifu! Kwa utukufu WANGU MIMI, YEHOVAH, kwa Utukufu wa MWANANGU YESHUA, na ROHO WANGU Mpendwa, kwa utukufu wa YAH!


Kwa hivyo hivi, hivi karibuni, yote yale dunia imepanda, itavuna pia. Wale wanaohuzunika sasa watafurahia baadaye. Wale wanaofurahia sasa, watahuzunika baadaye.


Hawakuchukulia kwa uzito onyo la Siku 3 za Giza linalokuja. [Wako] pole pole sana kusikiliza sauti ya Manabii WANGU, kwa hivyo NItakuwa pole pole kujibu maombi yao. Lakini NItakuwa upesi katika kuhukumu dunia kwa uovu wake na makanisa NIkiita wengi kwa toba.


Ni nini zaidi inabidi Ninene Mwanangu kwa Marekani? Ni nini zaidi inabidi NIseme? Maana NImevuka mipaka yote ili hili taifa lipumue pumzi lake la mwisho. Ni nini zaidi NItasema? Hukumu yaja! Hukumu tayari iko hapa!


Mwisho wa Neno

14 views

Recent Posts

See All
bottom of page