top of page

Unabii 78 “Kuweni Katika Umoja. Sulubisheni Miili Yenu!"


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 27 Desemba, 2019


Maandiko Husika


Yohana 14:6

YESHUA Akamwambia, “MIMI NDIMI njia, ukweli na uzima.

Yeyote hawezi kuja kwa BABA isipokuwa kupitia KWANGU.


Hosea 5:15

NItarudi tena mahali PANGU mpaka watakapokubali kosa lao.

Nao watautafuta uso WANGU; katika taabu yao wataNItafuta kwa bidii.


Ezekieli 33:11

Waambie, ‘Hakika kama MIMI NIishivyo, Asema BWANA YEHOVAH, SIfurahii kifo cha watu waovu, bali kwamba wageuke kutoka njia zao mbaya wapate kuishi. Geukeni! Geukeni kutoka njia zenu mbaya! Kwa nini mkafe, ee nyumba ya Israeli?’


Ujumbe wa Kinabii


Unyasi mmoja hautengezi konde la majani. Wala mti mmoja hautengezi msitu. Vivyo hivyo ilivyo nanyi. Mshumaa mmoja hautengezi menorah lakini tu wakati mko katika mapatano nyote mnakuja pamoja. Kwa hivyo NIpeni UTUKUFU kwa kuwaunganisha katika ROHO na UKWELI. NIpeni sifa. NInafanya maajabu mengi makuu kwa niaba yenu, ikianza na mbegu ya wokovu. Eneeni [kama matawi] kwa ajili YANGU. Acheni mizizi yenu ikue. Msizuie kazi ya ROHO MTAKATIFU (Yakobo 1:4). NIruhusuni NIwe MTUNZA BUSTANI wenu, kwa maana Nawapa pumziko. Nawapa amani (Yohana 14:27). Nawapa shalom.


MIMI ni YESHUA MILELE wa DAIMA. MIMI ni TUMAINI lenu la WOKOVU na KUHANI wa UFALME. NIfuateni katika njia za MELKIZEDEKI (Waibrania 7). NIfuateni MIMI katika utaratibu WANGU. MIMI ni utaratibu na sio vurumai za kuoza. NIfuateni katika njia ZANGU zote, watoto WANGU, na mtasitawi. Mtasitawi katika njia hamjui. Mtasitawi katika ROHO na katika UKWELI.


Lindeni mioyo yenu. Zuieni ndimi zenu kwa hatamu (Yakobo 1:26-27). Msiruhusu miili yenu iweke kando roho zenu. Tembeeni katika ROHO wa UTAKATIFU WANGU na hamtatimiza tamaa za mwili (Wagalatia 5:16). Ruhusini uhuishaji usitawi katika ardhi. MsiNIjaribu, watoto WANGU. Tembeeni mkono katika mkono, kwa maana wakati umekuja tai WANGU kuinuka – tai wa matawi saba. Kuna fumbo katika hili.


Fuateni njia za EZRA BABA yenu (1 Wakorintho 11:1). Mtumainieni na mkae katika kinga ya mabawa YAKE. Hili sio uabudu sanamu, maana yeye ni funiko lenu la maombi. Wakati mnaMtii, mnatii MIMI, YEHOVAH, kwa maana NIliMweka katikati yenu kuwa mwakilishaji WANGU, balozi WANGU wa upendo (2 Wakorintho 5:20). MsiMhuzunishe BABA yenu (Kutoka 20:12). Muonyesheni fadhili za upendo. Muonyesheni ukweli. Akisi YESHUA na muache kujificha katika mwili. Kuweni angavu kama bahari ya fuwele. Jitazameni mkisitawi na mjue kutokosa [kitu].


NIko hapa kuwabariki watoto WANGU, lakini tu mnapotii (Kumbukumbu 28:1-14). Wakati tu mkishika maagizo YANGU katika njia madhubuti kabisa. Nawapa nguvu. Nawapa nishati. NIna huruma juu yenu.


Mwisho wa Neno.

9 views

Recent Posts

See All
bottom of page