top of page

Unabii 86 “Wekeni Kando Njia Zenu [Kwa Ajili Ya] Njia ZANGU, Ee Israeli!


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 15-16 Februari, 2020

Maandiko HusikaMathayo 15:3

YESHUA Akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya MUNGU kwa ajili ya mapokeo yenu?


Yeremia 33:8

NItawatakasa dhambi zote walizofanya dhidi YANGU, na NItawasamehe dhambi zote za uasi dhidi YANGU.

Ujumbe wa Kinabii


Ee watoto WANGU warembo, sikizeni, tazameni, na mjifunze kutoka kwa BABA yenu METATRON. Kwa maana haangushi jasho kwa habari ambazo zinakuja KWAKE kutoka kushoto na kulia. Hana wasiwasi na Hahangaiki lakini daima Anaweka mtazamo WAKE mmoja, umekaziwa fokasi MIMI, YEHOVAH.

Nena, nena. Ita hukumu za “NDIMI NILIYE”, kwa maana ni za haki na kweli kama YULE AnaYEzipeana. MTAKATIFU wa Israeli na MPEANA-SHERIA wa pekee wa Sayuni (Isaya 33:22). Sikia, ee Israeli, na msujudu mbele ZANGU MIMI, YEHOVAH YULE wa MILELE wa ZAMA. Kwa muda mrefu mmekuwa kimya. Kwa muda mrefu sana mmeinamisha goti, lakini sio KWANGU. KWA muda mrefu sana mmedumisha njia za marabii wenu, mkichukua desturi na uongo za wanadamu badala ya Ukweli (Mathayo 15:1-9).


NIngependa mwe huru. NIngependa mjue “NDIMI NILIYE”. Wekeni kando vitabu vyenu na mje mNIjue. Njoni kwa “NDIMI NILIYE” MKUU. Njoni KWANGU na acheni NIwaoshe safi (Yeremia 33:8). Kazi zenu hazitawahi NIpendeza hadi mweke “NDIMI NILIYE” kwanza kwa kukubali MWANANGU YESHUA MASHIAKH wenu. YEYE ni MASHIAKH wenu na hakuna mwengine. Wengi NImetuma kwenu katika JINA LAKE na mmefanya nini? Mmewatupa? Mmewachukulia kama taka?


NInakutazama, ee Israeli. NInakutazama na mtazamo WANGU wa upendo, maana kwani wewe siwe tufaha la jicho LANGU [kipenzi CHANGU]? Lakini je si una mnyoo ndani yako? Ni mara ngapi lazima NIwaonye? Wakati mmoja anakuja katika jina lake, mnampokea. Lakini MIMI, mnakataa. Jinsi inavyohuzunisha. Ni machozi mangapi NImekulilia, Yerusalemu. Kwa muda gani hili litakaa? O jinsi unavyoNIhuzunisha, ee Israeli! Ndiyo, MIMI, YEHOVAH, NImehuzunika, NImehuzunika. O Israeli, NImehuzunika. Jinsi Alivyohuzunika NDIMI NILIYE!


Njoni KWANGU, ee Israeli. Je, hamuoni Navuruga maji kwa ajili yenu? Je, hamuoni Natuma watumishi WANGU kwenu, malaika WANGU wakuu? Kutana na Rafaeli. Kutana na Ragueli. Wawili WANGU, hawa wawili NItawatuma kwenu pia wale wengine. Kuweni tayari, ee Israeli, kwa maana hawa wawili, wawili WANGU hawaji kuburudishwa na dhambi yenu. Fikirieni kuhusu Sodoma na Gomorra. Fikiria jinsi malaika watakatifu walitumwa, jinsi walikuja (Mwanzo 19:1-27). Na nini waliona? Dhambi. Upotovu. Hukumu. Tahadhari, ee Israeli, kwa maana NDIMI NILIYE Hajafurahishwa.


Ee Tel Aviv, maendeleo ya kiteknolojia. . . MSIFIKIRI KWAMBA NDIMI NILIYE AMEFURAHISHWA. AU KUVUTIWA na kufanana kwenu. Njoni tu KWANGU na mtelekeze njia zenu za uovu. Telekezeni misimamo yenu ya kijinga. Chukueni Sodoma na Gomora kama mfano na muutilie maanani. Je, SIkuonya Korazini kutahadhari isije Sodoma na Gomora wainuke katika siku ya hukumu na kuwashutumu? Tahadharini isije Korazini iinuke na kuwashutumu (mathayo 11:20-24)!


Ee Yerusalemu, Yerusalemu njoo KWANGU. Fanywa upya katika DAMU YANGU. Tazama na ufanywe upya, kwa maana je, SIkuonya kuhusu zamu nne za saa za usiku? Uko wapi? NIlikutafuta katika ua la BABA YANGU bila mafanikio. Kwa maana hauko hapo. Hauko hapo. NIliita lakini haukuitikia. Je, si maksai yuajua hori la mmiliki wake (Isaya 1)? Mwasemaje? Nawawajibisha. Je, hamNIsikii au masikio yenu yamekuwa butu na kuwa mazito?

Mwisho wa Neno.

0 views

Recent Posts

See All
bottom of page