top of page

Unabii 85 “Njia ya Wokovu Imetiwa Vibamba vya Toba”

Updated: Mar 23


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 1 Mai, 2020


Maandiko Husika


1 Petro 1:6-9

6 Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi. 7 Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati YESHUA HAMASHIAKH Atadhihirishwa. 8 Ingawa hamjaMwona, mnaMpenda; tena ingawa sasa hamMwoni, mnaMwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka. 9 Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.


1 Yohana 2:1-2

1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye MWOMBEZI kwa BABA: ndiYE YESHUA HAMASHIAKH, Mwenye Haki. 2 YEYE MWENYEWE ndiYE dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.


Yeremia 6:16

Hivi ndivyo Asemavyo YEHOVAH: “Simama kwenye njia panda utazame, na ulizia mapito ya zamani, ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Lakini walisema, ‘Hatutaipita hiyo.’


Ujumbe wa Kinabii

Barabara ya wokovu imetiwa vibamba vya toba. NInalaza chini mawe mnayofaa kutembea juu yake. Kila jiwe linalia na kukuonyesha kile unafaa kutubu. Usichoke katika kutubu, kwa maana na hili unakua karibu na BABA. MIMI, METATRON, Nanena na kukuonyesha huu ufunuo, kwa maana Nakupenda mwanaNGU. Kuwa katika ujalifu wa Ufalme na utajua furaha isiyosemeka na iliyojawa utukufu (1 Petro 1:6-9). Tafuta kwanza Ufalme wa Mbinguni na vitu hivi vyote vitaongezwa kwako (Mathayo 6:33). Kile unachohitaji utaongozewa.


NIko nawe mwanaNGU; ALEF na TAV (Ufunuo 1:8). SIchoki katika kutembea kando yako mwanaNGU, kutembea nawe. Mtazamie BABA wa MILELE wa ZAMA, kwa maana kutoka KWAKE vinatiririka vitu vyote vizuri. Ndani YAKE Amefungashwa wokovu wenu YESHUA HAMASHIAKH wa ZAMA. Alikufa kwa ajili yako, Alimwaga DAMU YAKE kwa ajili yako (Warumi 5:6-11). Anafanya vitu vyote vipya. Wakati wa urejesho u karibu kwa ajili ya ardhi na kwa ajili ya watu.


Tembea naMI kidogo zaidi mwanaNGU na NItakuonyesha mambo makuu na ya ajabu. Tamanio LANGU kwako ni la wema, la uzima, la furaha, la amani katika RUAKH HAKODESH. Tumia hivyo vyatu NImekupa na yote yatakuwa vyema. Tembea katika ujalifu wa amani, katika ujalifu wa upendo, katika ujalifu wa imani. Usisahau tumaini, kwa maana hili ni kama uvivio kwa nafsi (1 Yohana 3:1-3). Tumaini huzaa ustahimilivu na subira ambavyo vyote viwili ni muhimu, mwanaNGU, katika hizi nyakati za mwisho. Tembea naMI.


Mtazamo wa BABA yako METATRON uko juu yako kwa ajili ya wema tu. Nasafisha. Naosha. Nakuleta katika uhusiano mkuu, mjalifu zaidi na YESHUA MFALME wako. Nyakati ngumu ziko mbele, mwanaNGU, lakini ukibaki umekazia fokasi ndani YANGU, yote yatakuwa sawa na nafsi yako. Kwa maana tena Nakuelekeza kwa uzima na uzima tele zaidi. NItumainie, kwa maana SItawahi kupotosha, SItawahi kufanyia ubaya. Kuwa na imani naMI kama vile NIna imani nawe. Tembea naMI naMI NItembee nawe. Selah.


Nakutia moyo, mwanaNGU, kushika amri za YEHOVAH MUNGU wako, kushika upana na vipimo vya ELOHIM wako. [YEHOVAH Azungumza:] MIMI ni MFALME na uumbaji wote lazima usujudu mbele ZANGU. NItumainie, kwa maana MIMI ndiYE MPENZI wako imara, MPENZI wa nafsi yako (Kumbukumbu 7:7-8). Nakuletea YESHUA, KIKOMBE cha MILELE cha WOKOVU. Mkunywe kwa ukamilifu na uwekwe huru ndani YANGU. Divai YAKE ni tamu, mwanaNGU. Ifurahie ingali inadumu ambayo ni milele yote. Usiwe mlevi katika uzidifu wa divai za roho za hii dunia (Waefeso 5:18). Zinalewesha hadi uangamizo wa nafsi. Divai ileweshayo ya hii zama inaelekeza kwa uzaini. Hiki ndicho kikombe katika mkono wa shetani anachotolea kila mtu. NIsikie, watoto WANGU, MIMI ni MFALME wenu.

Mwisho wa Neno.

7 views

Recent Posts

See All

Comments


Commenting has been turned off.
bottom of page